Ondoa haraka App ya Msomi Bora - Msomi Bora - Biashara

Latest

Friday, July 10, 2020

Ondoa haraka App ya Msomi Bora

                              

Ondoa haraka App ya Msomi Bora

App yetu kwa sasa haifai, na sio salama tena kwa matumizi
App hii ilikuwa imedukuliwa na kutekwa na wahalifu

- Wahalifu hawa walifanikiwa kuidukua na kuiteka hii app tokea Mwezi January 2020

- Tuliweka tangazo watu waiondoe hii app katika simu zao, na hatujawahi tena kiutangaza hii app katika blog yetu.

- Lakini wahalifu hawa walihakikisha app bado inabakia playstore, na watu bado walikuwa wanaendelea kuipakua hii app na kuitumia. 

Matokeo yake

App hii imewekewa virus na program ambazo zimepelekea majanga yafuatayo kwa watumiaji: 

1. Picha, taarifa na namba za simu za watumiaji wa hii app zaidi ya 1500, zimeibiwa na kusambazwa katika mitandao ya kijamii, na kutumika vibaya pasipo wao kujua zimefikaje huko.

2. Simu za watumiaji zaidi ya 1000 zimezima ghafla na hazikuwaka tena, mara baada ya kuitumia hii app kwa muda mrefu. 

3. Wahalifu wamekuwa wakiweka matangazo ya ngono katika hii app, baadhi ya wasomaji hutulalamikia sisi ndio tumeweka hayo matangazo.

4. Watumiaji wa hii app hawapati mambo yote ambayo tunaweka katika blog yetu ya Msomi Bora, kuna vitu vingi tu vinabadilishwa na kuondolewa kupitia hii app. 

Kwa Usalama zaidi

- Ondoa hii app mara moja katika simu yako

- Tunakuomba msomaji wetu usome kupitia blog yetu ya Msomi Bora

- Kusoma kupitia Blog yetu ndio usalama wenyewe, udukuzi kama huu hauwezi kamwe kufanyika kwenye blog.

Kwa sasa Timu yetu iko jikoni ikitengeneza app mpya na imara ambayo haiwezi tena chezewa na wahalifu

Tunakujali na tunakupenda Msomaji wetu

4 comments: